Jumamosi, 2 Februari 2013

MCH TIMOTH MWITA AANZISHA KANISA DAR LINAITWA CITY WORSHIP CENTER

 Pastor Timoth Mwita si jina geni kwa wadau wa injili na mashabiki wa matamasha kwa miaka kadha sasa alikuwa chuoni akisoma na amemaliza mwaka jana. wakati akiwa chuoni alikuwa chachu ya kusifu na kuabudu pale chuoni TAG Dodoma na aliwahi andaa Tamasha kubwa sana pale Dodoma lililojaza watu kwenye uwanja wa mpira wa Jamhuri. pia amekuwa akishiriki kuandaa mikutano mikubwa ya Injili kule kigoma na hata hapa Dar na amekuwa akitafsiri pia. na mwaka jana alilikuwa na mlolongo wa matamasha mengi yaliyokuwa yamepewa jina la New Season Double Grace ambayo nayo yalifanya vizuri sana.
Hapa ni kwenye moja mikutano mikubwa Kigoma

Tamasha kubwa lilojaza watu pale Dodoma kwenye uwanja wa jamhuli liliandaliwa na Mch Mwita


sasa amemaliza na sasa anaanzisha kanisa hapa Dar linaitwa City Worship Center na kwa sasa watakuwa wanasalia katika shule ya Sunrise iliyopo pale Morocco karibu na Hospital ya ARR. akiongea na blog hii amesema anawataka watu waje wamwabudu mungu katika roho na kweli na watu wataona jinsi Mungu anavyo onekana katika nyakati hizi alisema Ibada zitaanza Jumapili ya Tar 03/02/2013 kuanzia saa 09:00 - 11:00 asubuhi. na anakaribisha watu wote na waleteni na wagonjwa ili wakutane na nguvu za Mungu.

moja ya matasha mkubwa yaliyoandaliwa na Mch Mwita

Mch Mwita akikalimani moja ya mikutano mikubwa kule kigoma

unaweza wasiliana na mtumishi huyu kwa no 0784/0655461435

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni