Jumapili, 6 Januari 2013

WAIMBAJI WAKIKE WENGI WA INJILI WAAMUA KUJIKITA KATIKA UPIGAJI WA VYOMBO VYA MUZIKI

Mwimbaji Frola Mbasha akiimba huku akipiga kinanda
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mwamuko wa waimbaji wa kike kujifunza kupiga vyombo vya musiki tofauti na zamani ambapo kazi hiyo ilifanya na wanaume tu. Kwa kwetu Tanzania bado ni jambo geni ni wachache sana ambao wamepata mwamko huo hasa wale ambao wana tembea nchi nyingine na kuona wanawake wakipiga vyombo vya mziki tena kwa umahili mkubwa kama wanavyo fanya wanume.

Sarah Shilla mwimbaji wa nyimbo za injili
                                 
Nichukue nafasi hii kuwapongeza ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na juhudi ya kujifunza ala za mziki, kuna baadhi ya watu katika pita yangu humu mtandaoni nimeweza kuona juhudi zao katika picha walizoweka. Na kutokana na uzoefu wa upigaji vyombo mbalimbali nilionao ni rahisi kwangu kutambua mtu ambaye amepiga picha huku akiigiza kupiga vyombo hivyo tofauti na Yule ambaye anajua kupiga.

Neema mwimbaji wa nyimbo za ijili
Bado natoa changamoto kwa wanawake kuweza kujifunza mambo mbali mbali yanayofanya katika jamii kwani yanaweza kuwa ajira katika maisha yetu badala ya kuona kuwa jambo hili labda ni la wanaume au wanawake, wenzetu nchi zilizoendelea wamefanikiwa sana utakuta mwanamke anapiga dram kuliko hata mwana mme, au gita, keybord, na vyombo vingine vingi. Kama unayo nafasi jifunze na hata ikibidi kwenda kwenye vyuo maana siku hizi kuna vyuo vingi vya kufundisha mziki
Huyu ni Jane James akipiga gitaa Huyu ni Abby Malecela Mtoto wa Blogger ambaye hupenda kufanya kila kitu anachofanya baba yake hapa alikuwa na miaka 2 tu naamini atakuwa mpigaji wa vyombo huko baadae.

Wewe bado hujaanza unasubiri nini anza sasa.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni