Jumanne, 1 Januari 2013

MCH KANEMBA AANZA MWAKA KWA KUWAONGOZA WATANZNIA KUIOMBEA NCHI YA TANZANIA

Mch Dunstan Kanemba amewaongoza watanzania katika kuiombea nchi ya Tanzania. Alisema kuwa anaona Tanzania yenye mafanikio ijapo kwa sasa bado kunaonekana hakuna tumaini lakini anamwamini Mungu anaweza kufanya mambo makubwa katika nchi yetu kiuchumi na kiroho. Amewataka watanzania kutokukata tama ya maisha. Ijapo Tanzania sasa ina watu karibu million 45 haijalishi hata kama watu million 40 wakasimama na kulaani Tanzania. Na waliobakio million 4 waomba kwa Mungu aliyehai, Mungu anasema atasikia na kuponya nchi. Akinukuu andiko la 2Nyakati 7:14 Mungu anahitaji maombi ya watakatifu. Aliongeza kusema kuwa hatima ya Tanzania iko mikononi mwa watakat ifu na si viongozi watanzania wengi wamejisahau na kusubiri Tanzania iwafanyie wao na hilo ni kosa watu ndo tunatakiwa tufanye kitu kwaajili ya Taifa letu. Wananchi wametakiwa kujiamini katika msitakabari wa Tanzania, pamoja na wingi wa watu waliopo bado utajiri uliopo unaweza kubadilisha maisha ya watu wa Tanzania. Ikiwa watanzania wataamua kwa dhati kuibadilisha Tanzania itabadilika na kuwa kama nchi nyingine zilizoendelea.

Alisema kuwa kuna mambo makuu matatu yanayotesa watanzania kwa sasa 1 ni rushwa na rushwa itaondoka tu kama watanzania wote watapambana na rusha na si kuwaachia viongozi peke yao, twatakiwa kuendelea viongozi wanaofanya vizuri na zaidi ya yote tunatakiwa kuandaa viongozi waadilifu. 2 waandishi wa habari wamechangia sana kuharibu fahamu za watanzania kwa kuandika maovu tu na si mema ya taifa magazeti yote na vyombo vingi yamejaa picha mbaya na habari mbaya tu habari nzuri haziandikwi, alisema ijapo mema ni mendi lakini hayaandikwi wana baki kuandika habari wanazozitaka wao ili wapate pesa, huku wakiacha kizazi kinachokuwa na watu wengine kujua hakuna njema katika nchi yetu bali ni uharibifu tu, hivyo wanalijenga taifa lisilo na maadili maana yale mazuri hayaandikwi hivyo wana kosa pa kujifunza maana wana jua kuwa hakuna jema. 3 ni ukabaji uuaji, watu wengi hawaishi kwa jasho lao bali wamekuwa ni waporaji waibaji wa vitu vya wengine wana vyozalisha na hili limekuwa katika kila sehemu na limeharibu fahamu za watu na kujua kuwa hakuna kufanikiwa bila kuiba.

 Baada ya hapo aliongoza kuimba wimbo wa Taifa ambao uliimbwa na Praise team na kanisa lote kwa ujumla na baadae alimalizia na maombi maalumu ya kuiombea nchi , alitoa mfano wan chi za Indonesia ,Korea, China ambazo wananchi waliamua kwa dhati kubadilisha nchi zao na ikawa hata kwa Tanzania inawezekana aliongeza kusema tusilaumu waliopo madalakani ila tuwaombe sana.

zifuatazo ni picha mbalimbali za ibada hiyo
wanakwaya wa kwaya mbili wakiimba wimbo maalumu wa pamoja wa mwaka mpya kwaya hizo ni Dio-doxer walivaa nyekundu na kwaya ya Revival waliovaa kijani

Kwaya ya pamoja


washika mipini mpiga solo the blogger Martin mwenye tai nyekundu na mpiga bass mkongwer arstotile wapigaji wengine hawapo pichani

The blogger martin Malecela nikiwa na mke wangu

Hapa tukiwa na mtoto wetu Abby

Hapa the blogger nikiwa na Igwe Papaa Lumelezi akiwa ametoka ki nigeria na mimi ki america

Hapa papaa Lumelezi na mkewe wakiwa na Mchungaji kiongozi na mke wake Dunstani Kanemba

Wazee wa meza kubwa

Mr Mwakibuti wakitoa sadaka ya shukrani

gasper Lameki na mkewe wakimshukuru Mungu kwa kufanikisha harusi yao

Jerry Shija na mkewe wakimshukuru Mungu kwa kufanikisha harusi yao

Watoto nao walikuwepo hapa ni abby wakiwa na mess

Prise team ya kanisa wakiimba wimbo wa Taifa huku wamenyanyua bendela ya taifa juu wakiongozwa na mchungaji kiongozi
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Shower and alter your garments before you go to sleep every single night. Make sure to thoroughly hair shampoo the hair. This will likely take away the buildup of substances you acquire through the day. This too helps from dispersing substances, like dust particles and plant pollen, to your bed furniture and creating allergy symptoms a whole lot worse right away. [url=http://www.x21w12w21.info]Ho7ii340k[/url]