Alhamisi, 15 Novemba 2012

SARAH SHLLA ANAENDELEA NA UTENGENEZAJI WA VIDEO YA LET IT RAIN IN HIS PRESENCE, ITATOKA MAPEMA MWAKANI

 Wengi mtakumbuka uzinduzi uliofanywa miezi michache iliyopita na mwana dada mahili mwimbaji wa nyimbo za gospel Sarah Shilla. wa albamu yake ya let it rain in His presence.

albamu hiyo yenye nyimbo zipatazo 12 sasa video yake iko mbioni kukamilika. video hiyo inayorekodiwa katika viwango vya kimataifa huko india  itakuwa sokoni mapema mwakani. katika video hizo ameshirikiana na waafrika wengine kutoka nchi mbalimbali kama Leosotho ,Burundi Tanzania na Uganda na baadhi ya sehemu wamerekodia katika kanisa la Calvary lililoko huko India

Album hiyo imesheheni aina mbalimbali za muziki ili kuleta radha nzuri kwa watakao nunua, mahadhi hayo ni kama  zulu kwaito,rnb,rock,sebene na imeibwa kwa lugha ya kingereza kiswahili,na kizulu.

blog hii ambayo ilifanya mahojiano na mwimbaji huyo moja kwa moja kutoka India, ambaye yuko huko kwa muda sasa alimalizia kwa kusema kuwa watanzania wakae mkao wa kula kwani atakapo rudi hapa TZ atakuwa na ziara katika mikoa kadha ili kutambulisha video ya hiyo albamu yake mpya ambayo ni ya kwanza akiwa sehemu kubwa kaimba yeye mwenyewe. pamoja na kutengeneza video hiyo pia alisema audio cd za nyimbo hizo zipo madukani kwa yeyote anayehitaji anaweza kuzipata.


Maandalizi ya kuanza kazi

wakiangalia quality za picha za picha na kweka settings sawa


Kazi hii inahitaji umakini hasa inapokuwa ya kimataaifa jamaa hajajikunja bure ni ili kipatikane picha bora


Kazi kweli kweli

Action

Stand by

Wakipata maelekezo kutoka kwa director

Yes hapo poa haya tunaanza

Action

Mambo ya mapouda


Kazi kweli hasa mbele yako kunapokuwa na camera badala ya kundi la watuNgoja nije niwalekebise

Nyuma yacamera kila mtu yuko busy ili kuleta picha bora


Ni kazi ya kuchosha sana lakini itakamilika
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni