Ijumaa, 16 Novemba 2012

MASANJA MKANDAMIZAJI MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AMBAYE DVD ZAKE ZINAUZIKA KWA WINGI

Masanja mkandamizaji ndiyo jina linalojulikana na wengi lakini jina lake ni Emanuel Mgaya, ambaye anajulikana sana katika tasnia ya uchekeshaji hapa inchini lakini hivi karibuni ameibukia katika uimbaji wa nyimbo za injili baada ya kuokoka.


DVD hiyo inayobewa na wimbo unaoitwa hakuna jipya chini ya jua una nyimbo 8 ambazo zote ni kali kutokana na utunzi na uimbaji uliotumika. kwanza ina ujumbe ambao kila ambaye hajaokoka hawezi sema kuwa hajaelewa kwanini masanja kaokoka imekaa kiinjilisti kabisa pili kuna maneno ya comedi ndani yake ambayo yanasababisa kurudia kusikia na kufurahisha na kukuacha ukiwa na furaha tatu kuna mionekano mingi ya uchekeshaji ambayo inafurahisha na mwisho uchechaji ambao umepambwa na stage show wa flora mbasha unafanya dvd hii kuwa ya tofauti. kuna watu wengi ambao wameshiriki kwenye DVD hii tofauti na tunavyo ona DVD nyingine mwanzo mwisho muhusika ni yule yule baadhi ya walionekana ni shwahiba yake Silas Mbise, Frola Mbasha, Mc Regan, Sarah Mvungi, na wengine wengi kutoka kanisa la mito ya baraka.

ujio wa albamu yake ya gospel umewafanya watu wengi hasa asiyookoka kuwa na maswali juu yake naye kwenye nyimbo zake hakuucha kutoa majibu ya  maswali yao. katika nyimbo zake kama chapa mwendo, nimemchagua na maisha yangu ni majibu tosha ya maswali ya watu wote. Labda swali ambalo halikujibiwa kwenye DVD yake ni kuwa kaachana na kundi la ze comedy? yeye mwenyewe anajibu kuwa bado ataendelea kuchekesha mpaka hapo atakapo ambiwa na Mungu achane na kazi hiyo kwani hiyo ni kazi kama kazi zingine inamwingizia kipato, we unacheka yeye siku inaingia.Masanja ambaye sasa yuko busy katika shamba la Bwana kuliko hata huko the comedy ameeleza kuwa hawa wana komedi wenzake siku hizi hawashangai maana amekuwa na ratiba nyingi kiasi kwana akimaliza kuigiza ni mbiyo kwenda kutumika na hata simu yake imekuwa busy kupokea mialiko mbalimbali kwenda uimba kwenye matamasha na hata kwenye mikutano ya injili 
Masanja aliendelea kusema pamoja na kuwa na ze comedy lakini ana mpango wa kuanzisha christian comedy ili na watu wa upande wa pili wapate uhodo kwa kukitumia kipaji chake, na kazi hiyo imeshaanza kwa kushirikiana Emanuel Mbasha Mume wa Frola mbasha na muda si mrefu watu wataana kuona.
yeye peke yake ndiye aliyeokoka katika kundi zima la ze comedy anaendelea kumwomba Mungu awafumbue macho nao waone kile ambacho yeye ameshaona na wapendwa tunatakiwa tusaidi kwenye maombi hasa Joti anahitaji sana maombi alisema Masanja

ujio wa muimbaji huyu kwenye Gospel unaufanya muziki wa gospel kuzidi kupaa juu na kuizidi miziki mingine yote ya kidunia, na hii inatokana na kazi kubwa inayofanywa na waimbaji wa nyimbo za Injili ambao kwa kutumia vipaji walivyopewa na Mungu kwa sasa hata wasio wakristo wananunua na kusikiliza nyimbo za injili na shuguli nyingi siku za leo hata kama hakuna wakrito zinapigwa sana na ndo maana siku za leo siyo ajabu kuona nyimbo zinapigwa bar hiyo inaonyesha kuwa kila mtu anapenda kusikiliza nyimbo za injili
Wimbo wa chapa mwendo ambao Masanja ameshirikiana na Flora

Zaburi ya - - - -

Uje uje Emanuel - - - - -

Masanja katika wimbo wa niko busy


tangu nimeokoka mimimwenzako mambo yangu yamekuwa super siku hizi si pandi basi na kwea lipipa tu ni baadhi ya maneno yaliyoko kwenye wimbo wake wenye mahadhi ya bongo fleva .

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni