Alhamisi, 16 Agosti 2012

ROSE MUHANDO AKAMILISHA KUREKODI ALBAMU YAKE SOUTH AFRICA CHINI YA SONY

Yule malkia wa nyimbo za injili Tanzania Rose Mhando amemaliza kurekodi nyimbo zake mwisho wa wiki iliyopita South Afrika. kwa sasa mwanadada huyo yuko chini ya mkataba na kampuni kubwa ya muziki Duniani inayoitwa Sony. akizungumuza amesema ameshamalizia nyimbo 3 zilizokuwa zimebakia za albamu yake mpya na 2 za video.

wanadada huyo ambaye anatamba na albamu zake alizotoa huko nyuma kama Jipange sawa sawa, nibebe, Utamu wa Yesu nk. alipata mkataba huyo mwaka jana na sasa yuko na kampuni hiyo katika kutoa albamu yakee hiyo. Rose amabaye ni mzuri katika kutunga nyimbo na kutunga step ameweza kuguza mioyo ya watu sehemu mbalimbali Tanzania na nje ya Tanzania na kusababisha nyimbo zake kupigwa sana kwenye sherehe mbalimbali.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni