Jumanne, 21 Agosti 2012

MLOKOLE AFUNGWA MIAKA 2 JELA HUKO BAGAMOYO NI BINTI WA MIAKA 17 KOSA KABADILI DINI KUTOKA UISLAMU NA KUAMUA KUOKOKA.


Binti mmoja anayeitwa Eva Abdullah mwenye umri wa miaka 17 amehukumiwa jela miaka 2 kwa kubadilisha dini kutoka uislamu na kuwa mkristo. Binti huyo ambaye inasemekana alibadili dini miaka 3 iliyopita, alionywa na wazazi wake kuachana na kundi lililokuwa limemshuhudia na kuokoka na yeye alikataa na kuendelea kujitangaza kuwa ameokoka . Baada ya kukataa kuachana na ukristo, wakamuundia mastaka kuwa amekiuka  maagizo ya kitabu kitakatifu cha Quran. Na kesi ikapelekwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo hicho. Viongozi wengi  wa kikristo walishindwa kumtetea Eva kwenye vyombo vya sheria kutokana na mazingira ya uislamu wanayoishi huko Bagamoyo. Hivyo tar 26 July 2012 Eva akahukumiwa kifungo cha miaka 2 Jela.
Niliposoma habari hii mwili ulinisisimuka na kushangaa sana kuwa hili limetokea Tanzania mtu anafugwa kwaajili ya imani na sijajua kwa kifungu cha sheria ipi nimezoea kuona mambo kama haya yanatokea Irani, na nchi nyingi za uarabuni lakini si hapa kwetu Tanzania, kwa waraka huu naomba tuendelee kumwomba Mungu amtie nguvu na ujasiri ya kusonga mbele na kuendelea kuitangaza injili ya Bwana Yesu hata huko gerezani aliko. Binti huyu alitakiwa awe shule lakini yuko kifungoni tena si kama ameiba hapana ameokoka tu, unajisikiaje na je? Hatuna sheria ya kumtetea binti huyu ambaye mimi naona amenyimwa haki yake ya msingi ya uhuru wa kuabudu.  Mungu mkubwa kuwa binti huyo bado anaendelea na imani yake mbele za Yesu ijapo yuko katika mazingira hayo ya kifungo(2 peter 1:2-4) omba mungu ampe neema ya kuwashirikisha wengine neno la Mungu huko huko aliko.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Maoni 2 :

Unknown alisema ...

pazito hapa.ingekuwa Zanzibar ningeelewa ila na kwenyewe kwa wasiwasi; sasa hili limetokea huku Bara, kwanza nina wasiwasi na taaluma ya jaji mtoa hukumu na kama elimu yake iko sahihi basi kafanya jambo hili kwa makusudi. hii Tanganyika ni nchi isiyo na dini kama msingi wa mwasis wa taifa hili nyerere alivyosema(naichukia kauli hii) ila ZNZ ina dini;kitu pekee cha kufanya ni kumwombea dada huyu kwa kweli amakuwa sehemu ya kutimizwa unabii wa kuwa ametupwa gerezani kwa ajili ya jina la BWANA.

Nelson Faustin. alisema ...

inauma sana ndugu zangu, kwa ninachokiona baada ya miaka mitano ni matengano,kama hatutakaa vizuri na Mungu, itakuwa shida sana, ndugu zangu hawa siwalaumu ila, kuna mahali wanakosea sana, ni rahisi sana kwa wakristu kufanyiwa mambo ya ajabu tukakaa kimya than to a muslim, wasidhai hatuoni ila tunamjua tunaye Muamini...