Jumatano, 8 Agosti 2012

ASKOFU MKUU WA TAG ACHAGULIWA TENA KUONGOZA, MIAKA 10 YA MAVUNO KUENDELEA. BLOG HII INAMPA HONGERA KWA KUCHAGULIWA TENA

Mkutano wa kanisa laTANZANIA ASSEMBLIES OF GOD unaoendelea dodoma umemchagua
Barnabas Mtokambali katika nafasi ya uskofu mkuu kwa awamu nyingine. habari mpasuko zilizoifikia blog hii zinasema askofu huyo amepita kwa kura nyingi za 93 asilimia. kura za awali za maoni za kupendekeza zilionyesha dalili ya moja kwa moja kuwa anakubarika na asilimia kubwa ya wachungali.Barnabas Mtokambali

katika awamu iliyopita ameweza kufanya kazi kubwa ikiwapo kuliongoza kanisa hilo mara 2 ya idadi ya waumini waliokuwepo mwanzo pamoja na mambo mbalimbali, kwa kupita kwake inamaanisha kuwa kauli mbiu aliyoianzisha ya kuongeza kanisa itaendelea ya Miaka 10 ya Mavuno Tanzania kwa Yesu, Blog hii inachukua nafasi hii kupa hongera yeye pamoja na kanisa zima la TAG Tanzania.
Mchuano Mkubwa ulikuwa katika nafasi ya Makamu wa Askofu ambapo Dr. Muhiche alichuana vikali na Bishop Kameta katika kinyang'anyiro hicho Dr. Muhiche alifanikiwa kutetea kiti hicho kwa mara nyingine.
Pastor Ron Swai amechaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God kwa mara nyingine.


Kwa maana hiyo Viongozi wote wa Kamati Kuu Wamefanikiwa Kutetea nafasi zao kwa miaka minne mingine.

Akofu mkuu akitoa machozi ya shukrani

kesho utaendelea uchaguzi wa viongozi wa majimbo 
  KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni