Jumatatu, 18 Juni 2012

WAKRISTO NIGERIA WAENDELEA KULIA. JANA MAKANISA KADHAA YAMELIPULUWA NA MABOMU, WATU WAFAA NA WENGINE KUJERUHIWA.

wakrito wa Nigeria jana wameendelea kulia  tena baada ya makanisa kadhaa kulipuliwa na mabomu, sasa ni karibu mwezi ambako kumekuwa na milipuko katika makanisa kila jumapili, nilipuko ya jana inasadikika kuua watu 50 na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa. makanisa matatu yaliripotiwa kulipuliwa na mabomu jana nayo ni Shalom Chuch, ECWA church na Christ the King Cathedral. angalia picha zifuatazo.
Kanisa la Shalom lililolipuliwa jana

Bomu lilolipuliwa katika kanisa lililo eneo la zalia











Baadhi ya matukio ni
  1. Milipuko 3 imetokea Kaduna na mmojawapo ni katika kanisa la Shalom Chuch
  2. washirika wa  ECWA church walisema mlipuko ulitokea wakati mtu mmoja alipokuwa akilazimisha kuingia ndani ya geti la kanisa baada ya kuzuiwa na askari.
  3. msemaji mmoja Yushau Shuiabu Said kutoka Kaduna alisema wakati wakiendelea kuwahudumia watu waliolipuliwa eneo Wusasa na Sabon walisikia mlipuko mwingine maeneo ya Kaduna
  4. Meya wa Kaduna ametangaza amri ya kutotembea ovyo kwa muda wa masaa 24 mpaka hali itakapokuwa swali. lakini pamoja na hayo miliputo hiyo ya mabomu ilifanya vijana wa kikristo nao kuanza kufanya fujo hovyo mitaani nao wakachoma msikiti moja na kuubomoa mwingine
  5. kumelipotiwa kuwa watu 34 wamekufa na zaidi ya watu 156 kujeruhiwa huko Kaduna.
  6. Christ the King Cathedral kumeripotiwa watu 10 wamekufa na wengine 50 wamejeruhiwa.
  7. Dr. Lawal Khalid ambaye ni mkurugenzi wa ABU Teaching Hospital amethibitisha kuwa wamepokea watu 9 waliokufa na na kuna wengine 39 walishafikishwa awali na wengine wamekufa wakati wakipatiwa matibabu na wengine wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Wapendwa tuendelee kuwaombea wapendwa duniani kote ambao wako katika wakati mgumu wa machafuko yasiyosha na tusisahau kuomba kwaajiri ya nchi yetu pia haya yasitupate. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki afrika.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: