Jumatano, 27 Juni 2012

SINEMA YA YESU ILIYO MAARUFU, IMETAFSILIWA KATIKA LUGHA ZAIDI YA 1100 DUNIANI, WATU MILIONI 200 WAMEOKOKA KWA KUIANGALIA TU, IMEANGALIWA ZAIDI YA 6MILIONI, NDIYO INAYOONGOZA KWA KUANGALIWA NA WATU WENGI, ILITENGENEZWA KWA GHARAMA YA $ MILIONI 6Watu wengi tunajua au tumesha wahi kuuangalia mkanda wa Yesu. Mkanda ambao umebadilisha maisha ya watu wengi na kumwelekea Yesu, ni mkanda uliotafsiliwa katika Lugha nyingi kuliko yote zaidi ya lugha 1,100 duniani, na ina historia kwa uuzwaji wake na kuangaliwa na watu wengi sana duniani karibu mara billion 6. Na watu wapatao 200 milioni wamemfuata yesu na makanisa mengi kuanzishwa baada ya watu kuangalia mkanda huu. Sasa leo nakuletea historia fupi ya utengenezwaji wa mkanda huu na wakati mwingine nitakuletea historia fupi ya aliyeigiza nafasi ya Yesu ni bwana Brian Deacon.

Deacon ambaye aliigiza kama Yesu watu wengi huwa wanajua ni halisia siyo ya kuigiza hata wengi wakitokewa na Yesu kwenye maono huwa wanamuona kwa sura hii.


Mkanda wa filamu ya Yesu ulitengenezwa mwaka 1979 ambao unachukua uhalisia wa maisha ya Yesu kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Luka ndani ya kitabu cha Biblia. Walioongoza namna ya kuigiza ni Peter Sykes kutoka Australia , John Heyman na John Krisch hawa ni waingeleza na iliingiziwa katika nchi ya Israel.
Mawazo ya kutengeza mkanda huu yalianza waka 1945 kwa kijana mdogo mfanya biashara jina lake Bill Bright yeye alitaka kujitolea kughalamia utengenezaji wa mkanda huo, ambao ungewavutia watu na kuonyesha uhalisia wa kile kilichoelezwa kwenye biblia na ambao ungeweza kutafsiliwa katika Lugha nyingi. Lakini badala ya kutimiza hiyo azima yake Bright akaenda kutafuta kikundi cha huduma za kikristo ndipo atakutana na wanafunzi wa chuo ambao walikuwa wanajiita Campus Crusade for Christ mwaka 1951.mwaka 1976 Bright akiwa na Campus Crusade for Christ wazo lake la kutengeneza filamu ya maisha ya Yesu ilimrudia, na akapewa wazo kutafuta hela ili kuiweka biblia nzima kwenye filamu, wazo hilo alipewa na John Heyman ambaye alikuwa ni mwingeleza aliyezaliwa ujerumani akiwa producer  wa hollywood, lakini kutokana na ghalama kubwa za kuitengeneza wakaona watengene kitabu kimoja tu cha Luka. hivyo Campus Crusade walianza kuchangishana hela na kutafuta njia mbalimbali za kupata $6 million.
baada ya hapo team ya watu 500 ambao walikuwa ni wanachuo na viongozi wao kutoka katika vikundi vya kikristo na visivyo ya kikristo akaanza kufanya utafiti wa kina juu ya filamu hiyo itakavyo kuwa, na ikafuatiwa na mazoezi na mafunzo namna ya kuigiza kwa miezi kadhaa huko mashariki ya kati.(Israel)
hivyo basi utengenezaji ulianza na mtengenezaji mkuu alikuwa ni John Heyman ambaye alikuwa ni mwingeleza aliyezaliwa ujerumani na wakamtafuta mwigizaji Brian Deacon ili kuigiza nafasi ya Yesu, nafasi ya Mariamu iliigizwa na Rivka Neumann,Yusuph iliigizwa na Yosef Shiloach, na mwigizaji mwingine aliyehusika ni Paul Eshleman ambaye aliwahi kuongoza mkanda mwingine wa yesu kabla ya huu, yeye aliigiza kama askari wa kirumi juu ya farasi ijapo alikuwa anajua kirumi kidogo.

katika filamu hii ambayo Deacon aliigiza kama Yesu, ilimugusa sana nafasi yake ya kuigiza kama Yesu na ilimfanya asome aina mbalimbai za tafsili za Biblia ili kupata kile ambacho Yesu alimaanisha kwenye mafundisho yake, na Niko Nitai ambaye aliigiza kama Petro aliamua kuwa muumini wa Yesu kihalisia wakati wakiendelea na uigizaji wa sinema hiyo. baadhi ya maeneo yalitajwa kwenye Biblia kama mto yordani ambako inaaminika kuwa ndiko alikotoka Petro ndimo filamu hasa ilikoigiziwa.
baada ya muda filamu ilikamilika na ilibidi ipelekwe kwa wanavyuo wa Biblia ili kuiona, na watengenezaji walichukua tu kitabu cha Luka  badala ya kuchanganya vitabu vyote vya injili kama wengine walivyoshauri, baada ya kuangaliwa na kutolewa baadhi ya maoni ikaonekana ni vyema ibaki kwenye kitabu cha Luka tu hivyo filamu ya Yesu ikatolewa na kuonyeshwa mara ya kwanza na Warner Bros huko Marekani, pamoja na hayo haikuweza kurudisha hela ya ghalama iliyotengenezewa kwa wakati huo hivyo kukawa na hasara ya $2 milioni.
mwaka 1981, Bill Bright alianzisha mradi wa sinema ya Yesu na lengo lilikuwa kuitafsili sinema hivyo katika lugha mbalimbali na iweze kuonyesha kote duniani. na tafsili ya kwanza ya filamu hiyo ilikuwa ni kwa lugha ya Tagalog ambayo inatumika na wafilipino. wakaanza kuwatumia wamishenari duniani kote kuionyesha na kuisambaza sinema hiyo na hata kule ambako watu hawajawahi kuona sinema, wamepelekewa na kuiona na kwa marekani ilibidi filamu hii igawiwe makanisani na kila mtaa. na mwaka 2004 ikaanzishwa tovuti ambayo watu wanaweza kuangalia mkanda huu kwa lugha 300 tofauti, na kuna filamu yingine ya hadisi za Yesu kwa watoto ambayo iliigizwa na eacon pia inatatikana DVD na VHS na iko kwenye mradi huo pia.
http://www.inspirationalfilms.com/av/watch.html

 


Jesus
  
Directed by
Peter Sykes
John Krisch
John Heyman (uncredited)
Produced by
John Heyman
Richard F. Dalton
Written by
Barnet Bain
Luke (book)
Starring
Music by
Distributed by
Inspirational Films
Release date(s)
October 19, 1979 (US)
Running time
115 min.
Country
United Kingdom
Australia
United States
Language
English
Budget
$6 million

unaweza pia kusoma katika link hizi hapo chini
http://www.religion-online.org/showarticle.asp?title=2114

http://link.brightcove.com/services/player/bcpid78450078001?bckey=AQ~~,AAAAEau7i9k~,egPrrTuxsy9qzBZAqOiJHMep8d_MnwIX&bctid=993497674001
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: