Jumatatu, 18 Juni 2012

SAKATA LA UAMSHO Z'BAR LAIBUKIA BUNGENI


MBUNGE wa Ole, Zanzibar Bw. Rajabu Mbaruk Mohamed (CUF), amemtaka Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kutoa tamkoa la kuunda Tume Huru ambayo itafanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu waliosababisha vurugu zilizotokea hivi karibuni visiwani Zanzibar zikihusishwa na kundi la Uamsho.

Bw. Mohamed aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma juzi waakati akiuliza swali kwa Bw. Pinda na kudai kuwa yupo tayari kuunda tume huru iweze kufanya kazi na wahusika ili watakaobainika wachukuliwe hatua.
Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema Mei 26-27 mwaka huu, vurugu kubwa zilitokea Zanzibar zikihusishwa na kikundi kimoja kilichosajiliwa ili kueneza dini ya Kiisilam mwaka 2001 lakini kikaingia katika masuala mengine yasiyohusiana na dini hiyo.

Alisema kikundi hicho kilianza kupinga Muungano baada ya kuanza mchakato wa Katiba Mpya na kufanya maandamano ambayo polisi hawakuwa na taarifa nayo.
Bw. Pinda alisema, kikundi hicho kinapaswa kudhibitiwa ili kutoa fursa ya kufanikisha mchakato wa uandikaji Katiba Mpya kwani Serikali ikiachia jambo hili bila kuchukua hatua, kukundi hicho kinaweza kuleta madhara makubwa.

Aliongeza kuwa, kutokana na vurugu hizo baadhi ya watu waliohusika wamekamatwa akiwemo kiongozi wao mmoja ambaye ni Shekhe Juma Mussa Issa na kudai kuwa taarifa za kiusalama zinasema kikundi hicho hakitaki Muungano uliopo.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.