Jumamosi, 9 Juni 2012

MTOTO WA MIAKA MIWILI ALIYEKUFA, AFUFUKA NA KUKAA JUU YA JENEZA LAKE NA KUOMBA MAJI YA KUNYWA AKAFA TENA



MTOTO ALIYEKUFA NA KUFUFUKA NA AKAFA TENA
imeripotiwa kutoka Brazil.
Taarifa hii ni ya ajabu sana, na ningumu kuaminiwa, ORM alisema Kelvin Santon, alipoteza uwezo wa kupumua wakati akiwa kwenye matibabu ya ugonjwa ujulikanao kwa jina la pumu katika hospitali ya Belem, kaskazini mwa Brazili. Daktari wake anasema mtoto huyo alijulikana akiwa ameshakufa ilipo fika saa moja jioni, siku ya ijumaa, na mwili wa mtoto huyo uka kabidhiwa kwa familia yake ukiwa kwenye mfuko wa plastiki.

Familia ya mtoto huyo waliuchukua mwili wa mtoto huyo aliye kuwa tayari amefariki kuupeleka nyumbani, huku ndugu wakiomboleza kwa usiku mzima huku mwili wa mtoto huyo ukiwa umewekwa ndani ya jeneza lililokuwa wazi.

Saa moja kabla ya shughuli za kwenda kuuzika mwili wa mtoto huyo siku ya jumamosi, mtoto huyo akaamka akaoneka amekaa juu ya jeneza lake na akasema: “Baba naomba maji ya kunywa?” Baba wa mtoto, Bwana Antonio Santos, akasema kila mmoja alianza kupiga kelele, hatuamini macho yetu. Tulifikiri ni muujiza umetokea na mtoto wetu amekuwa hai tena. Kelvin akalala tena akarudia hali yake ya awali, hatukuweza kumuamsha kwani alikuwa ameshaaga kwa mara nyingine. Bwana Santos ambaye ni baba wa huyo mtoto alimkimbiza tena mtoto wake kwenye hospitali ijulikanayo kwa jina la Aberlardo Santos huko Belem Brazili, ambapo madakitari waliufanyia utafiti mwili wa mtoto huyo na kugundua kuwa tayari mtoto huyo amesha poteza maisha.

Baba wa mtoto huyo alisema: ‘Madakitari wali muhakikishia kuwa mtoto wake alikuwa tayari amekufa na hawakumpa maelezo yoyote kuhusu kile ambacho Baba wa mtoto huyo aliwaeleza hapo awali.’

Familia ya kijana huyo, walichelewa kufanya shughuli za maziko wakiwa na matumaini kuwa kijana wao anaweza akaamka tena, lakini hakuweza kuamka tena, wakaenda kuuzika mwili wa mtoto huyo muda wa saa kumi na moja jioni.
Baba, wa Kelvin katika picha akisema kuwa kifo cha kijana wake kimetokana na uzembe wa matibabu.

Bwana Santos, amefungua jarada la mashitaka katika moja ya kituo cha polisi, na polisi bado wanaendelea kufanya upelelezi zaidi kuhusu kifo cha mtoto huyo.

Alisema: ‘Baada ya dakika kumi na tano alipofika  katika hospitali hiyo kwa uchunguzi  zaidi ya ugonjwa wa mtoto huyo, madakitari wakamwambia kuwa kijana wake ameshakufa na wakamletea mwili wa mtoto wake. Akaongeza na kusema yamkini hawakumfanyi uchunguzi vizuri. Mtu alikuwa amekufa anaamka na kuanza kuongea, ukweli utabidi ujulikane.’


Taarifa zilizo tolewa ni kwamba idara husika ilithibitisha kuwa kijana huyo alipelekwa hospitalini akiwa mahututi, na  alifariki baada ya kuugua ugonjwa ujulikanao kitaalamu  kwa jina la  ‘cardiac-respiratory failure.’ Yaan kushindwa kwa mfumo wa upumuaji kufanya kazi.

siku zote shetani anashambulia sana watoto na hapendi kuona wanakuwa pamoja na matibu ambayo tunawapaitia watoto wetu lakini tunatakiwa pia tumuombe Mungu kwa ajili ya afya za familia zetu ili shetani asituonee.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.