Jumatatu, 18 Juni 2012

DVD MPYA YA NYIMBO ZA INJILI YA MASANJA MKANDAMIZAJI YAGOMBEWA JANGWANI!

Yule mchekeshaji maarufu Masanja mkandamizaji ambaye ametoa DVD yake ya nyimbo za injili yenye wimbo maarufu hakuna jipya chini ya jua. ambayo imetoka hivi karibuni inawezekana ndiyo DVD iliyokuwa inunuliwa kwa wingi wiki iliyopita pale Jangwani masanja ambaye nae alipata nafasi ya kuimba katika mkutano mkubwa wa injili uliomalizika jana jagwani kama ilivyo ada aliwavutia watu wengi, DVD hiyo ambayo haichoshi kuangalia, kila siku watu wakikuwa wakiikosa baada ya wauzaji kusema kuwa zimeisha mpaka kesho.


Album hiyo yenye nyimbo tisa, imerekodiwa maeneo tofauti nchini na nje ya nchi ambapo kazi ya kurekodi ilichukua muda mrefu na sasa imekamilika, ambapo audio yake kwa walioisikia wameikubali hasa uimbaji wa wawaitikiaji ambao wana sauti zilizojaa na mvuto huku Masanja mwenyewe a.k.a mchungaji mtarajiwa akijazia kwa mashairi mbalimbali ambayo licha ya mafunzo mazito pia inakuachia vicheko na tabasamu ikiwemo wimbo uliobeba album wenye maneno aliyochombeza kama Mungu akang'oa koki ya bomba mvua ikanyesha .... na maelezo mengine mbalimbali

Mwimbaji na mchekeshaji huyu pia anaimba kwaya ya New Jerusalem Choir (Watoto wa mito ya baraka) ya kanisa la E.A.GT Mito ya baraka lililochini ya askofu Bruno Mwakiborwa likiwa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam karibu na jengo la klabu ya soka ya Yanga.Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye album hiyo ni pamoja na Hakuna jipya, Nimemchagua, Maisha yangu, Chapa mwendo, Hili nalo litapita, Amini,Zaburi ya 150, Busy pamoja na Wadogo zangu(maalumu kwa watoto).

Kitu ambacho amewahi kuwachekesha watu kuhusiana na album yake hiyo, Masanja alisema anaruhusu wezi wa kazi za waimbaji kuiba watakavyo kwani wanamsaidia kutangaza injili na kumtangaza zaidi kwahiyo ikawa kama ametoa ruksa kwa wale wezi, jambo ambalo ni tofauti kwa waimbaji wengine ambao wamekuwa wakilalamika kuibiwa kazi zao kila leo

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: