Jumanne, 12 Juni 2012

ASKOFU WA TEF ATISHIWA KUAWA

Askofu wa kanisa la Tanzania Evangalism Field (TEF) la Shinyanga Edson Mwombeki amedai lipo kundi la watu wanaomtishia kumuua bila sababu za musingi. Mwombeki amedai kuwa watu hao wana mtishia kwa madai kuwa anawafuga vikongwe ambao ni wachawi na kwamba kwa sababu hiyo wanataka kumuua yeye pamoja na vikongwe hao.

alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. alisema mimi kweli ninao wanaume na wanawake wazee 23 ambao nawalea kwa kuwapatia chakula, malazi na mavazi ninayoyatafuta kutoka kwa wafadhili mbalimbali alisema. askofu huyo aliwataja watu watano wanaomtishia kumuua na kwamba tayari alisha ripoti polisi. akisimulia tukio la hivi karibuni alisema mmoja wa watu hao alifika kwenye eneo la kanisa lake na kuanza kutoa matusi kisha kuanza ugomvi na mtoto aliyemtaja kwa jina la Mlokozi (7). aliyepigwa na alisikia kilio cha mtoto na kutaka kujua kulikoni ndipo na yeye alipoanza kutukanwa.

anasema mtu huyo alitamka waziwazi kuwa watamuua maana anawafuga vikongwe ambao ni wachawi. baada ya kusikia hayo nilienda polisi na kuripoti na tayari polisi wanafuatilia suala hilo. Kamanda wa polisi mkoa Ndugu evarist Mangalla alithibitisha kupokea kwa taarifa hizo na kwamba wanaendelea na upelelezi ili kujua kwa undani. katika hatua nyingine Askofu Mwombeki amewataka watanzania kutii sheria za Mungu na nchi ili amani iweze kudumu, Mwombeki alisema Mungu anaipenda inch ambayo wananchi wake wana mtii yeye pia na kuheshimu mamlaka zilizowekwa madarakani. alisema Mungu anakataza uovu na kwamba binadamu hawana budi kuacha uovu ili waweze kuishi kwa amani.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni