Jumatatu, 2 Aprili 2012

ADHABU HII NI NDOGO ALIPA FAINI YA SH 6 MILION KWA KUWADHALILISHA WATOTO CHINI YA MIAKA 10!

Mtuhumiwa mmoja ambaye ni raia wa Uturuki ambaye alikuwa akifanya utalii nchini uganda Ndg Emin Baro ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 2 au alipe faini ya sh 6 mil. amelipa faini ya mil 6. mtuhumiwa huyu alikuwa antuhumiwa na kosa la kuwadhalilisha watoto wa kike kijinsia waliokuwa na umri wa chini ya miaka 10 huko nchini Uganda. ilidaiwa kuwa alikuwa akiwapiga picha hizo za uchi wa myana na kuziweka mtandaoni. raia huyo ambaye ni mwalimu nchini kwao. hapo utajiuliza kama mwl ambaye wazazi wanamwamini kumwachia watoto halafu anafanya vitendo hivi ni aibu. habari zaidi zimedai pamoja na kuwapiga picha watoto hao alifanya ngono na baadhi ya watoto hao na kuwaacha uchi na kuwachukua picha za video na kuweka katika mitandao mbalimbali.

wasichana hao ambao walikuwa zaidi ya 50 walikuwa na umri usiozidi miaka 10 jamaa huyo alikiri kuwapiga picha na kuzitumia katika mtandao. pamoja na kuwa tukio hili kutokea Uganda ndani ya Afrika mashariki lakini kumekuwa na matukio mengi ya wanawake kuzalilisha kijinsia hata hapa kwetu Tanzania na baadhi wa raia wa kigeni. zinatakiwa kuchuliwa hatua kali ili huu ushenzi wanaouleta katika nchi zetu ukome.

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni