Ijumaa, 30 Machi 2012

MGONJWA ALIYEPONYWA KWA KUFANYIWA MAOMBI AWASHANGAZA MADAKTARI

Njia za Mungu zi juu sana kuliliko njia zetu na mawazo yake ni juu sana kuliko mawazo yetu na ndiyo maana wakati mwingine anafanya vitu ambavyo hata akili zetu zinashindwa kuelewa. hivi karibuni dada Vicky masawe alikuwa anaumwa na kwenda hospitali kwaajiri ya matibabu na uchunguzi wa madaktali ulionyesha kuwa anamatatizo makubwa. kwanza aliambiwa kuwa kizazi chake kimegeuka, na alikuwa na uvimbe tumboni ambao alitakiwa afanyiwe upasuaji ili kuondoa uvimbe huo. na alikuwa na tatizo la ngozi yake pamoja na damu. na alikuwa ameshazuiwa kula chakula cha usiku ili kujianda na upasuaji huo lakini kabla ya upasuaji huo alienda kanisa la TAG Magomeni kwa Mch Kanemba akaeleza shida yake na kufanyiwa maombi na mwanamaombi Ayubu na baada ya maombi tu akawa mzima kabisa wakati huohuo. baada ya kupata uponyaji wake na kurudi nyumba ni akiwa mzima kabisa na kuwaeleza watu wa nyumbani kwake kuwa amepona. lakini baba mkwe wake hakukubaliana kabisa na kusema haiwezekani mtu kufanyiwa maombi na kupona.
Vick Masawe akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji katika kanisa la TAG Magomeni.

 kesho yake ilibidi baba mkwe alimweleza nilazima waende hospitali akaonane na daktali maana alitakiwa kwenda ijapo dada Vicky aliyepona alikataa lakini baadae ilibidi akubali ili kumrizisha mkwe wake na wakaondoka na kwenda hospitalini kwaajili ya matibabu na mkwewe akasema kama kweli ikithibitika kuwa amepona basi na yeye ataokoka. baada ya kufika hospitali wakaonana na Dr lakini alishangwazwa kuona kuwa mgonjwa ambaye alikuwa anategemewa kufanyiwa upasuaji, anamwambia kuwa yeye si mgonjwa tena ameponywa na Yesu. dr hakukubali na akjua mgonjwa wake ugonjwa umeongezeka maana anaeleza kitu ambacho kwa akili ya kibinadamu haiwezekani baada ya mjadala ilibidi dr agize vipimo viludiwe upya ili kuthibitisha usemi wa mgonjwa wake na walianza kipimo kimoja kimoja mpaka kipimo cha mwisho,! kweli alikuwa amepona ila dr hakukubali ilibidi amhoji vizuri mgonjwa wake maana si jambo la kawaida. lakini baadaye ilibidi Dr akubali kuwa inawezekana mtu kupona kwa kufanyiwa maombi maana iliwahi kutokea tena mtu kama huyu aliwahi kusema nae ammepona baada ya kufanyiwa maombi.
Hiki ni cheti alichoandikiwa na msululu wa magonjwa
Dr akiwa ameweka x baada ya kupima mara ya pili na kuona kwa kweli mgonjwa amepona
Cheti cha mara ya pili kinachoonyesha kuwa mgonjwa kapona kabisa.

Mumewake ndugu Masawe akionyesha vyeti vinavyoonyesha vipimo kabla na baada ya maombi.


Dr ilimchanganya sana lakini ilibidi akubali maana alisema vipimo vyao wanaviamini na zoezi la vipimo alisimamia yeye mwenyewe hivyo ni sahihi mgonjwa amepona. jina la Bwana libalikiwe kwa matendo yake makuu. ndungu yangu kama unaumwa ugonjwa wowote ule ukiwa mahali popote waone kanisa lolote la watu waliokoka ili ufanyiwe maombi na utapona kabisa asilimia kubwa ya magongwa yanasababisha na nguvu za giza.

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.

Hakuna maoni: