Jumatatu, 23 Januari 2012

ALBAM MPYA YA GOSPEL NITANG'ARA





NAWASALIMU KATIKA JINA LA BWANA YESU KRISTO


Namshukuru Mungu wetu kwa kutuamsha wazima siku ya leo. Nachukua nafasi hii kuwaeleza tena juu wa ujio wa albamu yangu ya Nitang’ara tu ambayo ipo katika mfumo wa CD.



Kwa wasionifahamu naitwa Mwinjilisti Kabula J.George. Namtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na hii ni albamu yangu ya tatu. Albamu yangu kwanza ilijulikana kwa jina Amani niliitoa mwaka 20...05.



Albamu hiyo haikuwa na ubora nikaamua kuifanyia marekebisho ni kachukua baadhi ya nyimbo nikairekodi upya na jina nikaibadilisha nikaiita ‘PESA’ huo ulikuwa mwaka 2007.



Alibamu hiyo iliingia sokoni na ilifanya vizuri sokoni. Mwaka 2009 nilifanikiwa kurekodi albamu ya pili iliyojulikana kwa jina la Ushindi.

Ndani ya albamu hiyo kulikuwa na wimbo wa Dhihirisha ambao ulifanyika msaada mkubwa kwa watu wengi walifanikiwa kuisikiliza na kuiona kwani yenyewe nilifanikiwa kuifanyia video.



Namshukuru Mungu anayenipa pumzi mwaka 11 nikafanikiwa kutoa albamu yangu hii ya Nitang’ara ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.



Albamu hii ina nyimbo sita ambazo zimefanyika faraja kubwa kwa watu mbalimbali waliofanikiwa kuisikiliza kupitia Wapo Radio na Praise Power.



Nimeona ni bora kila siku niwe naelezea wimbo mmoja mmoja na leo naelezea wimbo wa Nitang’ara.



Wimbo huu niliupata baada ya kupita katika maisha magumu yaliyosababisha baadhi ya majirani zangu kunibeza kutokana na changamoto nilizokuwa nazipitia.



Nimepita katika nyumba mbalimbali ambazo majirani walikuwa hawaishi kunibeza. Nikiwa katika hali ya kuutafakari uweza wa Mungu kwa kuona kama ameniacha ndipo nilipopata wimbo huo.



Wimbo huo niliupata kutokana na kuongeza juhudi za maombi kwa kuamini kuwa siku moja nitang’ara licha ya kupita katika changamoto hizo ambazo wamekuwa wakizipata watu mbalimbali hasa wanaoishi kwenye nyumba za kupanga.



Kupitia wimbo huo, nimekuwa nikipata simu mbalimbali za kuupongeza wimbo huo kwani umegusa maisha hali ya wanayoishi na licha ya kupita katika changamoto hizo wanaamini siku moja watang’ara kwani Mungu wanayemuomba ni Mungu wa majibu.



Kwa leo niishie hapa kwa undani zaidi ya kile nilichokiomba kwa mungozo ya Roho Mtakatifu nakuomba ujipatie nakala yako siku itakapotoka naamini nawe utabarikiwa na itakupa matumaini zaidi ya kile unachokifanya hata kama kinaonekana hakiwezekani siku moja kitawezekana na kung’ara.See more

.
Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.

Hakuna maoni: