Ijumaa, 30 Desemba 2011

Mwaka umeisha una jipi jipya ulilofanya? jipange sawa sawa mwakani 2012. no 3

                  leo namalizia yale niliyokuwa nimeaanza wiki iliyopita kuhusu mambo mbali mbali ambayo yaliweza kutokea katika mwaka huu ambao umebakiza siku 1 kuisha na kuukaribisha mwaka mpya wa 2012. kuna matukio ambayo niliyataja awali na leo nitamalizia kwa mengine, katika mwaka huu kumekuwa na machapisho mengi sana yanayohusu freemason (kundi la waabudu shetani) ambapo zamani habari hizi zilikuwa adimu sana lakini kwa sasa karibu magazeti si chini ya 5 yamekuwa yakitoa habari zao sijajuaa ni habari zinavuja kutoka katika kundi hilo au ni njia ya wao kujitangaza kwa watu taratibu ili watu wasiwashangae na kumekuwa na uvumi mkubwa wa watu wengi maarufu wafanyabiashara na wanasiasa kuwa ni wafuasi wa kundi hilo la waabudu shetani ijapo hakuna hata mmoja ambae amekiri hadharani kuwa yeye ni mwabudu shetani. katika mzunguko wa mambo hayo ya kidini ikumbukwe kuwa ilitangazwa kuwa Mei 212011 ndio ungekuwa mwisho wa dunia nalo hilo liliteka hisia za watu wengi duniani na ninamshukuru Mungu kuwa nalo hilo lilipita, na kutoka katika makala mbali mbali za hao freemasoni wameonyesha kuwa tar 21 Dec 2012 utakuwa mwisho wa Dunia na mwisho huu sio wa kurudi kwa kristo bali taratibu nyingi tunazofuata kwa sasa zitakoma na kuanzishwa kwa utaratibu mpya yani New world order. tusubili tuyaone. tukio lingine ni la kuuliwa kwa watu waliokuwa machachali duniani wakwanza ni gaidi la kimataifa si mwingine ila ni Osama bin ladeni aliyeuliwa na makomando wa marekani, na mwingine ni raisi wa wananchi wa Libya Gadafi aliyeuliwa kwa aibu ndani ya nchi yake.

Osama kabla na baada ya kufa
 
Gaddafi raisi wa Libya aliyeuwawa mwaka huu
lakini kuna maandamano yaliyoendeshwa katika nchi mbali mbali katika pande za kaskazini mwa afrika na kuwatoa maraisi wao kwa nguvu (people's power) akiwamo raisi wa Misri Mubarak na wengineo wengi.
Hossen Mubarak wa Misri aliyeondolewa madarakani na nguvu ya umma.
      kwa kweli mwaka ulikuwa na mambo mengi ambayo si rahisi kuyaweka hapa yote nimalizie na mabo mawili la kwanza ni la muuziza aliotendewa rafiki yetu na si mwingine bali Prosper mtoto wa mtume Mwakitalima ambaye kwa kweli kwa akili za kibinadamu si rahisi kuamini kuwa mtu ametola salama kwenye ajari ile tena bila hata kuvunjika mfupa hata mmoja zaidi ya michibuko aliyoipata. hii utukufu apewe Mungu mwenyewe kwa ulinzi anao wapa watoto wake kila itwapo leo. na lingine ni hili lililotokea hivi karibuni la mafuriko yaliyotokea Dar na kuua watu wanaokaribia kama 50 na kuacha idadi ya watu kama 4000 hivi wakiwa hawana makazi ya uhakika na kupewa hifadhi kwa ndugu na jamaa na wengine na serikali yetu ni jambo ambalo halikutegemewa na nashukuru Mungu kuwa lilitokea mchana kama lingetokea usiku ingekuwa habari nyingine, bado Mungu yeye ni wa kutumainiwa na kuabudiwa milele yote kwa yale anayoyafanya katika maisha yetu. mwakni nitakuletea shuhuda halisi za wale walio kubwa na mafuriko katika kanisa letu la magomeni usikose.

Gari ya Prosper baada ya ajari

Mtoto wa Mtume Prosper akiwa katika pozi

gari ya Prosper na mwenyewe akiwa amekandamizwa na gari kubwa kwa muda kama nusu saa hivi lakini Mungu wa miujiza alimwokoa.


Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko(Jangwani)
    ni malizie tu kwa kukushukuru wewe mdau  na msomaji wa blog hii najua kama kungekuwa hakuna wa kusoma ningevunjika moyo lakini kwa sababu wapo watu wanao soma basi nami nitaendelea kuandika tu ili kupeana taarifa na changamoto mbalimbali katika safari yetu ya kwenda mbinnguni jambo la muhimu marufuku kukata tamaa hata kama malengo uliyoweka mwaka huu hayajaenda kama ulivyokusudi kaa chini tafakari harafu tafuta njia ya kutimiza malengo yako usikubari kushindwa kwani walioweza wana nini na wewe ushindwe una nini yale yaliyokusababisha ushindwe yawe ni changamoto  (Steeping stone) ya wewe kusonga mbele.

Nakutakia heri ya mwaka mpya 2012 wenye mafaanikio tele na tumwombe Mungu tuuone waka wote pamoja katika mafanikio Amen.

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni