Ijumaa, 5 Februari 2016

USIIPITE BILA KUSOMA, ONGEZA UELEWA. JINSI MITUME NA WANAFUNZI WA YESU KRISTO WALIVYOKUFA.

     
1. Mathayo.
Huyu alikuwa mkusanya kodi (mtoza ushuru) kabla ya kumfuata Yesu. Huyu ndiye alieandika kitabu cha Mathayo Mtakatifu. Alihubiri na kusambaza neno la Mungu huko Persia na Ethiopia ya sasa. Aliuawa kwa upanga baada ya kuonyesha imani kali juu ya kanisa la kristo.

2. Marco
Huyu pia aliandika kitabu cha injili kiitwacho Marco Mtakatifu. Alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishoe alifariki.

3. Luka
Huyu ndiye alieandika Injili ya Luka Mtakatifu, mbali na kuhubiri neno la Mungu alikuwa ni tabibu pia tuseme kama msalaba mwekundu wanavyofanya. Alinyongwa mwaka 84 baada ya Kristo (AD) huko Ugiriki, hii ni kutokana nà msimamo wake mkali aliouonesha juu ya ukristo.

4. Yohana
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, Italia ya sasa. Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa. Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama askofu huko Edessa Uturuki ya sasa. Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. Petro
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisurubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusurubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba. Hii ni kwa ombi lake yeye mwényéwé hakutaka kusurubiwa kama Yesu.

6. Yakobo
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga kristo (mnara huo ni kama ule ambao shetani alimjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe). Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, maadui walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. James mwana wa Zebedayo
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa, James alichinjwa huko Jerusalemu. Maajabu ni kwamba askar aliyekuwa akimlinda gerezani alishikwa na mshangao jinsi James alivyoshikiria msimamo wake wa kanisa wakati wa hukumu. Baadae yule askari alienda akapiga magoti mbele ya James na kikiri imani yake mpya juu ya kristo. Wote walichinjwa mbele ya kadamnasi ya watu.

8. Bartholomeo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Asia ya sasa. Alimshuhudia Yesu kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa baada ya kugoma kuacha mafundisho yake ya kanisa.

9. Andrea
Aliuawa kama Petro. Kifo cha msalaba miguu juu kichwa chini. Ila maajabu baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua.

10. Thomasi
Huyu alihubiri neno la Mungu huko Syria, China na baadae India. Huko India alianzisha kanisa liitwalo Mar Thoma. Kanisa hili lipo mpaka leo huko India.
Aliuwa kwa kupigwa na mshale na askari wanne huko huko India kutokana na msimamo wake thabiti katika kristo.

11. Yuda (sio eskariote)
Nae pia alipigwa na mshale.

12. Mathias
Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda eskariote msaliti. Huyu alipigwa na mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

13. Paulo
Aliteswa na baadae akachinjwa na mfalme Nero huko Roma tarehe 9 mwezi june mwaka 68 Ano Domino (A.D). Ila mfalme Nero nae alijiua mwaka huo huo. Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua(waraka) nyingi kwa makanisa ya Roma. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

Inawezekana hii ni kumbusho kwetu kwamba mateso tunayopitia ni madogo sana ukiringanisha na haya ambayo mitume waliyapitia. Yote ni kwa ajili ya kutetea kanisa la Mungu. Ajabu siku hizi watu wamegeuza dini ya kikristo kuwa sehemu ya upigaji wa hela kutoka kwa masikini.

Naruhusiwa kurekebishwa kama kuna sehemu si sahihi. Na mimi ni binadamu.
"Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:22

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.