B
|
logger anayefanya
vizuri katika Tasnia ya Habari Za Kikristo, Uncle James Temu ambaye pia ni
Mtangazaji wa Kipindi Cha Rise and Shine na Sunday Special Kutoka Praise Power
FM na Mmiliki na mwendeshaji wa Blog ya
ameandaa siku maalum ya Kumshukuru Mungu kwa Blog yake Kutimiza Mwaka mmoja
Mpaka Sasa.
Uncle Jimmy
ameeleza kuwa blog hiyo ambayo mwezi huu wa July imetimiza Mwaka imepiga hatua
kubwa sana mpaka sasa katika upashaji wa habari ndani na nje ya
Tanzania.
Blog hiyo ambayo
ni maalum kwa ajili ya kupasha habari za Kikristo na injili imekuwa ikisomwa na
watu mbali mbali walio ndani na nje ya Tanzania kwa kipindi cha Mwaka mzima sasa
na kutoa michango yao ya mawazo kwa maendeleo ya Blog
hiyo.
Mwanahabari huyo
James Temu au Uncle Jimmy amesema siku ya tarehe 20 July, 2012 kuanzia saa 1
usiku mpaka saa 3 usiku ameandaa Event Ya Kumshukuru Mungu itakayofanyika katika
hotel ya Tamal maeneo ya Mwenge. Katika event hiyo Kutakuwa na Wanamuziki Wa
Injili wanaovuma hapa nchini wakiongozwa na Dar-es-Salaam Band, Kutakuwa na
Vinywaji pamoja na Chakula kitakachopatikana katika
event.
Uncle Jimmy
amesema Event hiyo haitakuwa na Kiingilio sababu ni siku maalum ya Kumshukuru
Mungu. Pia alitoa mwito wa Kuwakaribisha Watu wote Bureeeeeeeeeeeee kabisa
Bureeeeeeeeee kuweza Kuhudhuria Cocktail Thanks Giving Ya Blog hiyo inayotimiza
Mwaka.
Kumbuka ni tarehe
20 July, 2012, Saa 1-3 Usiku, Kiingilio ni Bure, Kutakuwa na Live Bands,
Wanamuziki wa Injili, Wacheza Filamu Mbalimbali, Watangazaji wa Radio,
Wasikilizaji wa Radio na Wewe Msomaji pia Unakaribishwa kwa ajili ya Siku ya
tarehe 20 July, 2012.
D
|
on’t Plan To Miss
It.!
Kwa Hisani Kubwa ya www.unclejimmytemu.blogspot.com
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.