Alhamisi, 14 Juni 2012

STARA THOMAS BAADA YA KULALAMIKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI JOHN SHABANI AMJIBU

Utakumbuka kuwa wiki iliyopita mwanamziki wa Injili Stara Thomas ambaye ameokoka na kuacha kuimba mziki wa kidunia alilalamika kuwa wanamziki wa gospel hawampi support ya kutosha. akimujibu Stara,  John Shabani ambaye pia ni kiongozi wa chama cha muziki wa injili Tanzania  alisema atapata support ya kutosha wala asihofu, maana wao ndiyo kazi yao aliongeza kusema kuwa wao wanafurahi wanapoona wanamziki wanaokoka na kuamua kumwimbia Mungu, na kazi yao kama chama kuwa kila mwimbaji amutukuze Mungu kwa njia ya nyimbo. akizungumza mbele ya waziri wa Habari, vijana utamaduni na michezo Dr Fenella Mkangara alisema wamesha fanya hivyo kwa wanamziki wengi kama akina Chidumule, Mzee makasi na wengine wengi.

John Shabani akiongelea swala la Stara Thomas

Cosmas Chidumule akiimba
 hayo yalizungumzwa katika Tamasha lililo andaliwa na John shabani katika kanisa la TAG Magomeni. Stara Thomas nae alipewa nafasi ya kusema machache na aliimba wimbo, waimbaji wengine ambao waliwahi kuimba kwenye bendi za duniani na wakaokoka alikuwepo Chidumule na Mzee makasi ambao kila mtu alimba na Chidumule alitumia ukongwe kwenye fani hivyo kwa nyimbo zake mpya huku akiwa amejifua vyema kwenye upande wa kulitawala jukwaa tofauti na huko nyuma. John shabani aliweza kukusanya waimbaji wengi sana ambao siku hiyo waliimba akiwepo Upendo Kirailo ambae alitumia kipaji chake na sauti yake kwa kuimba live wimbo wa zindonga ambao ulisababisha ukumbi wote kuchangamka. wengine alikuwepo Faraja Ntaboba, Victor Haron, Stella Joeli, Kwaya ya Joybrigers mikocheni B, kwaya ya Revival Magomeni. NK.
Stara Thomas akicheza

Mzee Makassy Akiimba

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.