Jumatano, 27 Juni 2012

SERIKALI YAWATAKA WAIMBAJI WA INJILI WAJIUNGE NA CHAMA CHAO ILI WAWE NA NGUVU YA PAMOJA, PIA MAKAMPUNI YA SIMU YAFADHILI MATAMASHA YA GOSPEL

Waimbaji wa nyimbo za Injili  wametakiwa kujiunga na chama chao cha mziki wa injili ili wawe na nguvu ya pamoja katika kudai haki zao. hayo yamesemwa na waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Dr Fenela Mkangala, huku akisema kuwa serikali itaendelea kufuatilia ili kuhakikisha watu wananufaika na kazi zao na kutokana na gharama kubwa za kuanda matamasha waziri ameomba makampuni ya simuna mengine yajitokeze kudhamini matamasha haya ya nyimbo za injili maana hata huku wanaweza kutangaza biashara zao na kupata soko na kuweza kuongeza wigo wa ajira. aidha waziri aliongeza kuwa atafuatilia kujua kwanini mirahaba yao inazereweshwa na cosota.

Dr Fenela Mkangala


Hotuba ya waziri wa by martmalecela http://soundcloud.com/martmalecela/hotuba-ya-waziri-wa/s-uIA1D




hayo aliyazungumza wakati akizindua blog ya kikristo ya John Shabani Magomeni TAG



KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.