Alhamisi, 28 Juni 2012

MWANAMZIKI MAARUFU WA GOSPEL DON MOEN KUZURU TANZANIA KWA MARA YA KWANZA, CHRISTINA SHUSHO NA THE VOICE KUIMBA NAE JUKWAA MOJA


Yule mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili kutoka Marekani Don Moen atakanyaga Tanzania kwa mara ya kwanza mwezi Agosti 11-12 katika viwanja vya jangwani. Don ambaye ana nyimbo zinazoimbwa Duniani kote kama God he will make way, Give thanks na nyingine nyingi, zimemfanya kupata umaarufu mkubwa Duniani kote na kuzunguka karibu nchi mbalimbali kumhubiri Kristo kwa njia ya nyimbo http://martmalecela.blogspot.com/2012/03/pata-historia-fupi-ya-don-moen-mtinzi.html . Don ataimba katika tamasha litakalo fanyikia katika viwanja vya jangwani  bonyeza hapa  http://lovetanzaniafestival.com/get-involved/ 
ambalo litafanyika katika viwanja vya Jangwani Dar. waimbaji wa kitanzania ambao wataimba pamoja na Don kwenye jukwaa moja ni mwimbaji mahili Christina Shusho na The voice mwimbaji mwingine maarufu atakuwa ni Nicole C. Mullen bonyeza hapa  Nicole C. Mullen na Dave Lubben. ikumbukwe kuwa miaka miwili iliyopita mwimbaji mwingine wa Injili kutoka Marekani Ron Kenoly  naye alidhulu Tanzania na aliimba kwenye viwanja vya Jangwani pia. soma histori yake hapa http://martmalecela.blogspot.com/2012/02/jua-history-ya-mwimbaji-maarufu-wa.html

Taarifa nilizozipata kuwa tamasha hilo litahusisha michezo mbalimbali na mtu yeyote ambae ana uwezo wa kuonyesha mchezo wowote basi aende akajiandikishe kwenye kanisa la Azania front  Tar 7 kuanzia saa 4 asubuhi.

na maelezo mengine zaidi unaweza kuangalia clip hizo hapo chini.



Stunt Dudes Ramp Shows! from Action Sports Outreach on Vimeo.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.