Tuni
Parata ambaye anafanya kazi katika hotel ya SkyCity nchini New zeland ameshinda
kesi juu ya boss wake ambaye alikuwa akimzuia kuwa na biblia sehemu ya kazi, kibali
hicho kimepatikana baada ya kikao na boss wake huyo.
|
Tuni Parata akiwa na biblia yake ndogo aliyokutwa nayo |
Ms Parata
akutana meneja wa mchana wa leo baada ya baada ya kuandikia barua ya kujibu kuonekana
akiwa na biblia sehemu ya kazi kitu
ambacho hakiruhusiwi kwenye kasino hiyo kitendo ambacho kingeweza kumfukuzisha
kazi. Katika kikao hicho imeonekana kubeba biblia
siyo utovu na nidhamu na ametakiwa aendelee kubeba biblia yake ili mradi tu iko
kwenye pochi yake na anaweza kuisoma wakati wa mapumuziko.
Nimefurahisha
na kikao hichi na nimeruhusiwa kuendelea kuja na biblia yangu, alisema ms
Parata huku akionyesha uso wa furaha.
Mkurugenzi
wa Unite Union national Mike Treen nae alishangazwa na uamuzi uliokuwa
umechuliwa na hoteli ya SkyCity had haukuwa na umuhimu wowote.
|
akifurahi baada ya kuruhusiwa kuwa nayo hapa yuko na Mchunhaji wake |
Awali mama
huyo alituhumiwa kwa kosa la kukutwa na biblia kwenye pochi yake ambapo
walisema ni kinyume cha utaratibu wa kazi wa hoteli hiyo, wengine walisema kuwa
huwa anasoma biblia yake akiwa kaunta na kusababisha hata wateja kuondoka maana
wengine hawapendi kuona kitabu hicho. Pamoja na tuhuma hizo zilizokuwa
zinamkabili mama huyo ambaye amekuwa mfanyakazi wa hoteli hiyo kwa miaka 16
sasa. Aliwajibu kwa kusema kuwa hawezi kuishi bila hiyo biblia maana imekuwa ni
sehemu ya maisha yake. Na alikuwa tayari hoteli ichukue hakua kali ikiwapo hata
kufukuzwa kazi lakini si kuachana na biblia yake.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.