Jumatatu, 18 Juni 2012

MKUTANO WA JANGWANI JANA UMEISHA KWA KISHINDO WATU WENGI WAOKOKA, WATU WAFUNGULIWA KUTOKA NGUVU ZA SHETANI, WAHUDUMU WAWA NA KAZI KUBWA YA KUHUDUMIA MAELFU YA WATU WALIOHUDHULIA, WAZUNGU WALIOKUWEPO WAJIFUNZA KISWAHILI KWA BIDII

Mkutano mkubwa wa injili ambao ulianza kuanzia Jtano ya wiki iliyopita jana umekwisha kwa kishindo baada ya umati mkubwa kuhudhulia, watu walikuwa wengi na pamoja na hilo kulikuwa na burudani ya kutosha kutoka kwa waimbaji mbalimbali, pamoja na bandi ya SOS kutoka swedeni ambao waliimba nyimbo kadhaa za kiswahili kama, e-baba e-baba e-baba pokea sifa, na ule wimbo maarufu wa Rose Mhando wa Bwana Yesu eeeh nakupenda. sijajua nani kawafundisha lakini waliimba vizuri utafikiri wana mda mrefu hapa Tanzania. wapiga vyombo waliokuwako jukwaani kwa kweli ni wataalamu sana na ilivutia sana pale walipokuwa wanawapigia waimbaji live bila chenga. kulikuwa na ile timu ya wazungu wanaokaribia 200 hivi nao kwa siku ya jana niliona wengi wakitamka maneno mengi ya kiswahili wakati wakikaribisha watu kwenye mkutano kama Bwana asifiwe, jambo, Karibu sana, Mungu akubariki n.k. ukiacha mahudhulio makubwa ya watu pia walikuwepo wachungaji kutoka katika makanisa mbalimbali ya hapa Dar. hata askofu mkuu wa TAG Dr Barnabas Mtokambali alikuwepo na ndiye aliyetoa nenola kumkaribisha mhubiri. katika maelezo yake alisema kuwa Duniani kuna madhehebu mengi sana ila mbinguni hakuna dhehebu tunatambulika kwa damu ya Yesu tu, alishukuru ushirikiano ulioonyweshwa na makanisa ya Kipentekste na kusisitiza kuwa umoja huo uendelee maana sisi ni watoto wa baba mmoja.

nilipata nafasi ya kuongea na mhudumu mmoja aliniambia kuwa watu waliofunguliwa ni wengi na waliokua wanaangushwa na mapepo ni wengi sana kiasi kwamba hata wanamaombi wahakutosha ilibidi kila mtu mmoja aombee mtu mmoja na wengine kukosa hata watu wa kuwaombea kutokana na wingi wa watu. baada ya mkutano huo kwisha maelfu ya watu waliookoka sasa wanatakiwa kuhudhulia semina ambayo inaendelea katika kanisa la Mito ya baraka kwa wale wote waliookoka jangwani.

baadhi ya picha za matukio.

















KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.