Jumatatu, 25 Juni 2012

KWETU PAZURI WATOA DVD MPYA ILIZINDULIWA DAR HIVI KARIBUNI


Kwaya ya nyimbo za Injili ya Ambassador of Christ kutoka kanisa la Wasabato wa Remera la jijini Kigali , imezindua albamu mpya iitwayo 'Mtegemee Yesu'.

Uzinduzi huo ulifanyika kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam. Nyimbo zinazounda albamu hiyo ni 'JY Ushime Uwite', 'Ndifuza Kugerayo', 'Iyana Iby'Isi', 'Yesu Niwe Mugenzi', 'Parapanda', 'Abasaruzi', 'Nenda' na huo wa 'Mtegemee Yesu' uliobeba jina la albamu.

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na uuzwaji wa DVD zenye nyimbo za albamu hiyo ambapo zilichangamkiwa na watu mbalimbali wanaohudhuria kwenye mikutano hiyo iliyopewa jina la 'Mwayachunguza Maandiko'.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mwenyekiti wa kwaya hiyo, Reuben Muvinyi alisema kuwa hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa kwaya yake kufanya uzinduzi wa albamu jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwaka jana walizindua albamu ya 'Kwetu Pazuri' kwenye viwanja vya Sabasaba na kisha Desemba mwaka huo huo wakarudi kuzundua albamu ya 'Twapaswa Kushukuru'.

"Sasa tumekuja tena Tanzania kwenye mikutano ya Injili lakini pia tumepata nafasi ya kuzindua albamu yetu mpya ya 'Mtegemee Yesu' ambayo tunaamini kwamba mtaipokea vizuri," alisema Muvunyi.

Aliongeza kuwa kinawasukuma kuja mara kwa mara Tanzania ni kutokana na ukarimu wa Watanzania na hivyo kadri Mungu atakavyowajalia wataendelea kuja kwa kuwa tayari wameshajenga urafiki wa kudumu.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.