Jumapili, 3 Juni 2012

BENNY HINNY BAADA YA KUISHI MIAKA KADHAA MBALI NA MKE WAKE SASA KURUDIANA, FAMILIA IMEFURAHI HARUSI KUFUNGWA MWEZI WA 12, MUNGU ALIWATENGANISHA MAKUSUDI! BENNY ALIKUWA KARIBU SANA NA HUDUMA KULIKO FAMILIA YAKE

Benny Hinn



Benny na Suzan

Benny na Suzanne Hinn aliyekuwa mkewe, baada ya kuachana kwa muda mrefu, vihi karibuni Benny Hinn ametoa ushahidi kuwa Mungu ni Mungu wa urejesho.
Wakati akiwa  Marekani  kwenye mkutano wa miujiza  uliofanyika alhamisi usiku tar 31 May, Benny Hinn alitangaza kuwa amefanya mapatano ya kurudiana na mke wake, Suzanne.
“Mchungaji Benny aliwaambia usiku ule” Maurice Sklar muanzilishi wa huduma ya Maurice Sklar, aliiweka habari hii kwenye ukurasa wa facebook. “kuwa Benny na Suzanne wamepatana! Benny alisema kuwa watafunga pingu za maisha kwa mara nyingine mwezi wa kumi na mbili! Maurice  anasema alivyosikia habari hiyo nusura aanguke kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia. Hakika huyu ni Mungu wa maajabu, alisema HUU NI MUUJIZA! Bwana Yesu asifiwe, nina furaha kubwa sana kusikia habari hizi!”
Baada ya miaka zaidi ya 30 ya ndoa, Suzanne aliomba apewe hati ya kuachwa ( taraka) mwezi wa Februari 2010 akikataa kuendeleza mahusiano yao kutokana na kutofautiana. Kwa wakati huo Benny Hinn alitoa taraka akisema “Nimeshitushwa na kufadhahishwa na habari hii sikuwa na taarifa yeyote ya awali”
Pamoja na kurejesha mahusiano yao, Suzanne alishangazwa kusikia habari ya tarehe yao ya kufunga ndoa kwa mara nyingine. Haya yalisemwa na ndugu wa karibu na familia hiyo katika kituo cha habari cha Charisma, “Tangazo hili lilikuwa ni la awali, lakini endelea kuliombea jambo hili,”
Baada ya Suzanne kujaza hati ya kuachwa, Benny Hinn alikiri kuwa amechangia kwa kufa kwa ndoa hiyo kwa kuwa karibu sana na huduma yake kuliko familia. Alisema kuwa mara nyingi nilikuwa nafanya huduma ya kuhubiri kwanza, nikitambua fika mafundisho niliyokuwa nafundisha yalikuwa yakiwaumiza watoto wake.
Hii ni habari njema nikijua kuwa itakuongezea Baraka na kukutia moyo katika familia yako. Mungu wetu ni Mungu uhuisho na matengenezo. Msalaba ni alama kubwa ya kuonyesha na kudhihirisha kuwa yeye ni Mungu anaye wapatanisha watu, na ndilo tumaini pekee la uponyanyi wetu. Nafahamu, kwakuwa ninauzoefu na uponyaji tangu nilipo yakabidhi maisha yangu kwa Yesu kwa miaka mingi iliyopita; lakini nimekuwa nikiufahamu mguso wa uponyaji wake kwa kipindi cha sasa alipoanza kuuonyesha utukufu wa uponyaji wake katika familia yangu, katika hatua za kuiuhisha ndoa yangu. Na uponyaji huu ulianza tangu sikukuu ya Krisimasi.....haikuwa krisimasi ya kuwa mpweke, maisha yangu yalibadilika kitofauti kuliko ilivyokuwa awali. Watoto wangu, wajukuu, na Suzanne kwa pamoja tulikutana siku ya krisimasi. Nilianza kuhisi kuwa Mungu ameanza kutembea katikati ya familia yangu nakuleta uponyaji wa uhuisho kwa maombi niliyo omba kwa muda mrefu. Tulicheka pamoja, kubadilishana zawadi, na kukumbushana maajabu mengi yakifamilia kwa miaka iliyopita, na niliomba maombi mepesi, “Bwana Yesu ilinde familia yangu kwa utukufu wa jina lako.” Kama wengiwenu mnavyofahamu, mke wangu, Suzanne tumekuwa na kipindi kigumu sana katika maisha yetu ya ndoa. Siku jiandaa kutangaza kwa kile kinachotaka kutokea, lakini na waombeni endeleeni kuiombea familia yangu, na pia endeleeni kuangalia kipindi cha televisheni cha Hii ni siku yako kwa habari ambazo Mungu atafanya.
Lakini nitaeendelea kusema, ninacho hitaji zaidi kuliko chochote ni mapenzi ya Mungu yafanyike katika maisha yangu, maisha ya Suzanne, kwa watoto wangu, na kwa wajukuu wangu. Kama familia tumekuwa mbalimbali  sana, lakini tumemuona Mungu akiwaita binti zangu kumtumikia, kumuokoa kijana wangu, na sasa yuko kwenye hatua ya kuhuisha ndoa yangu.

Wapendwa wangu naomba niwaambie kwamba kuhubiri injili ya Yesu ni moyo wangu, na ndo maisha yangu, na ninataka niendelee kuhubiri mpaka pale mapigo ya moyo wangu yatakapo koma. Nataka niliseme neno, “Yesu anaokoa, Yesu anaokoa, Yesu anaokoa” mpaka moyo wangu utakapo koma, kwa utukufu wa jina lake. Mmekuwa marafiki na ndugu zangu kwa kipindi chote, kwa yote yaliyotokea, kwa moyo wangu wote nasema asante, asante, asante. Pia namshukuru Mungu wangu kwa kuwaleta wote katika maisha yangu, nianomba awabariki  zaidi na zaidi, awape yote mnayo hotaji katika maisha yenu. Nina wombeeni kila siku, Mungu aponye maisha yenu, vyanzo vya fedha.

Endelea kuomba pamoja name kwamba kazi ya uponyaji wa familia yangu ukamilike, na haraka sana tutafurahi pamoja kwa lile atakalo lifanya Mungu. Nawapenda sana sana, ninyi ni watu wapekee kwangu naweza sema.



KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Maoni 2 :

  1. Hakika hii ni habari njema sana. Tena ni injili tosha. Mungu azidi kuwasaidia ili hila za mwovu shetani zibomoke vipandevipande na kutoweka kabisa kwa jina la Yesu!

    JibuFuta
  2. Habari njema sana, Mungu azidi kuonekana katika yote wanayotarajia

    JibuFuta

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.