Alhamisi, 31 Mei 2012

ASKOFU DAVID OYEDEPO WA NIGERIA, AKATAA KUMCHAPA MAKOFI MMOJA WA WAUMINI WAKE.

Askofu David Oyedepo
Billionaire mwanzilishi wa The living Faith Christian Church International, Askofu David Oyedepo, Aliyeanzisha sheria ya kuchapa washirika makofi hasa vijana pindi watakapo julikana kuwa ni wachawi. Askofu huyo amekanusha habari hizo hivi karibuni  yeye alishamchapa muumini wake makofi, taarifa za awali zinasema askofu huyo alimchapa makofi mmoja wa washirika wake, Baada ya tendo hilo mwanasheria mmoja akafungua kesi kwa niaba ya binti aliye chapwa makofi na Askofu huyo wakati wa ibada, mwanasheria huyo alisema Askofu huyo alienda kinyume, amekiuka haki za msingi za binadamu kama vile kusikilizwa, na pia amemvunjia heshima binti huyo.

Mwanasheria huyo aliiomba mahakama kumpa adhabu Askofu huyo kwa  kutoa jumla ya sh billioni mbili za Kinaigeria kama mfano na kumlazimisha Askofu huyo kuomba msamaha wa umma na katika magazeti ya kila siku na katika televisheni ya nchi hiyo.
Mwanasheria wa kanisa hilo alisema kuwa yeye na washiriki hawawezi kumshitaki, Askofu Oyedepo kutokana na misingi ya sheria la kanisa lao, lakini  wanasheria walibainisha kwamba kwasababu ya kukiukwa kwa haki za kimsingi za binadamu ilimpasa atiwe hatiani.

Awali ya hapo Askofu huyo alisha wahi  kuwasilisha sheria hii ya kuchapa makofi waumini  katika kanisa lake kuwa ni kitendo cha kudhibiti uharibifu ndani ya kanisa katika,  Sura ya 4 ya Katiba ya mwaka 1999 na Mkataba wa Afrika, Askofu huyo alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kumshitaki yeye wa hata mmoja wa waumini wake  


Desemba mwaka jana, video ya YouTube ilionyesha Askofu Oyedepo viciously akimchapa makofi msichana ambaye alikiri kwamba alikuwa "mchawi " wakati wa ibada alipokuwa amepiga magoti mbele ya madhabahu ya kanisa hilo. Video ya pili ilionyesha Askofu kuhalalisha hatua yake na kuongeza kwamba  huduma yake ni  "huduma ya  kofi" na kwamba "kama atapatikana mchawi yeyote atalazimika kumcha makofi mchawi huyo.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela


      Habari hizi kwa sasa zimeenea sana kwenye vyombo vya habari nchini Nigeria

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.