Jumamosi, 28 Januari 2017

SIKU zako ziwe NYINGI na UFANIKIWE



 Image result for mafanikio

Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako” (Kumbukumbu la Torati 5:16). Siku zako kuongezwa na kufanikiwa katika mambo yako, kwa ujumla tunaweza kuita hiyo ni baraka.

Kuwaheshimu wazazi (baba na mama yako) ni AMRI.

Maana halisi ya AMRI ni AGIZO ambalo likikiukwa kuna ADHABU. Ukisikia amri maana yake huna UCHAGUZI wa kufanya KINYUME na AMRI hiyo.
Katika KUWAHESHIMU baba na mama, kuna mtihani mkubwa kwa maana HESHIMA haipimwi na ATOAYE ila APOKEAYE. Hata ujitahidi vipi, kama “roho” ya apokeaye hiyo heshima HAIKURIDHIKA na kiwango cha heshima hiyo, bado haihesabiki kwakwe kama heshima hata kama umejitahida sana.

Nimekutana na watu wakidai wanawaheshimu wenzao ilihali wenzao wanalalamika hawaheshimiwi! Katika kutafakari sana maana halisi ya heshima, na sababu za kujua kama mtu amekuheshimu au la, nikakutana na mistati hii:
1 Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa. 2Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu. 3Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; 4ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa” (Mwanzo 27:1-4).
 
Isaka anasema, “ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa”, maana yake ni kwamba, kuna NAMNA ambayo (ile) MTU akifanya jambo, ROHO ya yule aliyefanyiwa inatoa baraka! Baraka hazitoki mdomoni; japo zinapita mdomoni.

Sasa angalia, imekupasa kujua namna “ILE” ya kuwafanyia wazazi wako mambo fulani ili “roho zao zikubariki”. Mtihani huu ni wa kila mtu pekeyake kabisa. Kila mzazi anahitaji vitu fulani kwa NAMNA ya tofauti na mzazi mwingine. Ili upate hizi baraka za wazazi wako, imekupasa KUFANYA sawasawa na WAPENDAVYO.

Kazi ya hizi baraka za wazai ni mbili: KUZIDISHIA umri wako na KUFANIKISHA mambo yako (kukustawisha).

Kumbuka jambo hili, wazazi wako wapo kwa kitambo tu, hunao siku zote. Kama wapo, usiwe mvivu, maana ipo siku utatamani kuwafanyia kitu na kumbe! Hawapo.

Frank P. SethKAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: